Kanali ya televisheni ya al Alam imeripoti kuwa, wananchi wa Saudi Arabia wana misimamo tofauti kuhusu hukumu iliyotolewa na vyombo vya serikali ya kutiwa nguvuni Mashia 23 kwa sababu ya kushiriki kwenye maandamano dhidi ya serikali katika eneo la Alsharqiyya.
Muungano huo umesema: Mashia hao 23 ambao wametambuliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia kuwa ni wahalifu na imetoa hukumu ya kutiwa kwao nguvuni, ni sehemu ya jamii ya Mashia wa Saudi Arabia ambao wanataka kurejeshewa haki zao zilizoghusubiwa.
Muungano wa Watu Huru umesema, tuhuma zilizotolewa na utawala wa Aal Saud dhidi ya raia hao ni za bandia na za kidhalimu.
Muungano huo umewataka wakazi wa Qatif kushiriki kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Zilzala ya Watu Huru yatakayofanyika Ijumaa ijayo kwa ajili ya kuonyesha malalamiko yao dhidi ya hatua hiyo ya serikali ya Saudi Arabia. 928852