Vyombo vya Habari vimeripoti kuwa Sheikh wa al Azhar Ahmad Tayyib aliitisha kikao hicho kwa lengo la kuchunguza mjadala ulioanzishwa na kamisheni ya marekebisho ya sheria ya 103 makhsusi kwa ajili ya kupanga upya shughuli za kituo hicho cha Kiislamu.
Wajumbe wa Kituo cha Kiislamu cha al Azhar walitoa maoni na mitazamo yao kuhusu sheria ya marekebisho ya sheria hiyo.
Mwanzoni mwa mwaka uliopita Sheikh wa al Azhar alibuni kamisheni ya sheria kwa ajili ya kuratibu upya kazi za Kituo cha Kiislamu cha al Azhar na taasisi zake.
Sheria mpya ya al Azhar imebuniwa kwa lengo la kudhamini kujitegemea kifedha na kiidara kituo hicho na kuunda baraza la maulamaa wa al Azhar litakaloshirikisha wanazuoni kutoka Misri na nchi mbalimbali duniani. Shekhe mpya wa al Azhar atateuliwa na baraza hilo ambalo litabuni sheria ngumu mno kwa ajili ya wanachama wake.
Tovuti ya al Wafdi ya Misri imeripoti kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo mpya, sheikh wa al Azhar Ahmad Tayyib atabakia katika nafasi hiyo hadi atakapofariki dunia. 929045