Polisi mjini humo wamesema tayari wameshamtia mbaroni aliyehusika na hujuma hiyo lakini Waislamu wanasema polisi wamechangia kuongezeka chuki dhidi ya Waislamu.
Hivi karibuni bomu la moto lilirushwa ndani ya Msikiti wa Kituo cha Kiislamu cha Imam Al Khoei wakati Waislamu 80 wakiwa ndani.
"Hatutavumilia tukio hili", amesema Meya wa New York Michael Bloomberg baada ya kukutana na wawakilishi wa Waislamu, Mayahudi na Wakristo katika Kituo cha Kiislamu cha Imam Al Khoei.
Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu CAIR limelaani vikali hujuma ya bomu dhidi ya msikiti mmoja huko New York wakati Waislamu wakiswali ndani ya msikiti huo.
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kumeshuhudiwa hujuma dhidi ya misikiti katika maeneo kama vile Massachusetts, Oregon, Ohio, New York, Iowa, Maine, Georgia, Missouri, Louisiana, Tennessee, Texas, California, na Michigan.
928956