Mkutano huo umeandaliwa na vijana Waislamu waishio Uhispania kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Waislamu wa Uhispania. Zaidi ya wawakilishi 70 wa vijana Waislamu nchini humo walishiriki katika kikao hicho ambapo wamejadili masuala ya kisiasa, kijamii na kisiasa ya Waislamu waliowachache mjini Madrid na miji mingine ya Uhispania.
Kikao hicho pia kilijumuisha iitikafu iliyoanza Jumamosi Disemba 31 na kumalizika Januari Mosi.
Kuna karibu Waislamu milioni moja nchini Uhispania ambao ni asilimia 2 ya idadi ya watu katika nchi hiyo ya Ulaya.
Uislamu una historia ndefu nchini Uhispani na wakati moja nchi hiyo ilitawaliwa na Waislamu.
929083