IQNA

Askari wa Israel washambulia msikiti wa al Aqsa

11:54 - January 09, 2012
Habari ID: 2253842
Taasisi ya Wakfu na Turathi za al Aqsa (AFEH) imeripoti kuwa askari wa utawala haramu wa Israel wameshambulia Msikiti wa al Aqsa na kupiga doria katika uwanja wa eneo hilo tukufu.
Tovuti ya Palestine Info imeripoti kuwa, taasisi ya AFEH imesema askari 10 wa utawala ghasibu wa Israel wakiwa pamoja na maafisa wa upelelezi wa utawala huo waliingia katika Msikiti wa Al Aqsa kwa ghafla chini ya ulinzi mkali. Askari hao wa Kizayuni wamekuwa wakivamia msikiti huo huo mara kwa mara lakini si kwa mtindo uliutomiwa mara hii.
Taasisi ta Wakfu na Turathi za al Aqsa imetangaza kuwa tukio hili ni hatari kubwa inayoashiria habari mbaya.
Ripoti zinasema kuwa utawala haramu wa Israel umeanza kuchimba mashimo mapya kusini mwa Msikiti wa al Aqsa katika eneo la Salwan kwa kisingizio cha kutafuta ukuta wa kale wa kihistoria. 931700

captcha