IQNA

Waislamu wa Bangkok waandamana kupinga uhasama dhidi ya vazi la hijabu

20:48 - January 10, 2012
Habari ID: 2255030
Mamia ya Waislamu wa Bangkok huko Thailand wameandamana mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo wakipinga kitendo cha walimu wa shule moja nchini humo kumzuia mwanafunzi mmoja wa Kiislamu kuvaa vazi la stara la hijabu.
Kundi la Waislamu kwa Ajili ya Amani limetangaza katika maandamano hayo kwamba kitendo hicho cha kuzuiwa vazi la hijabu kinaakisi chuki na uhasama dhidi ya Uislamu.
Kitendo hicho pia kinapingana na sheria za Wizara ya Elimu ya Thailand inayowapa Waislamu wa kike haki ya kuvaa hijabu mashuleni.
Taarifa ya kundi hjilo imesema baadhi ya walimu wa shule hiyo wamekuwa wakijizuia kumfunza binti huyo anayevaa hijabu wa Kiislamu.
Waislamu hao wa Thailand wamemtaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuingilia kati na kutatua kadhia hiyo. 933058


captcha