Amesema kwa masikitiko kuwa jumuiya hiyo imepuuza kabisa suala la Palestina kuwa kadhia muhimu katika ulimwengu wa Kiarabu.
Kwa mujibu wa gazeti la Tishrin linalochapishwa Syria, Muffti Sheikh Ahmad Badru Deen Hassun wa nchi hiyo amesema kwamba Jumuiya ya Kiarabu imeelekeza nguvu zake zote nchini Syria na kughafilika na suala muhimu la Palestina ambalo ni suala nyeti katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu.
Mufti wa Hassun amehoji ni kwa nini jumuiya hiyo imekuwa ikiandaa vikao vya dharura kujadili suala la Syria na wakati huohuo kughafilika na njama za utawala haramu wa Israel za kutaka kuyahudisha Quds Tukfu?
Ameshangaa ni kwa nini jumuiya hiyo haijachukua msimamo wowote wa maana dhidi ya tangazo lililotolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Israel kuwa Quds ni mji mkuu wa taifa la Mayahudi na Israel. Amehoji ni kwa nini Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Kiarabu wamekuwa wakifanya vikao vya mara kwa mara kuhusiana na Syria na kusahau kadhia ya Palestina?
Huku akisisitiza umuhimu wa kulindwa utukufu wa misikiti katika Uislamu, Sheikh Hassun ameitaka jumuiya hiyo pamoja na Umoja wa Mataifa kubadili msimamo wao kuhusu Syria. 932598