Vitabu hivyo vinavyosambazwa na wafuasi pamoja na vibaraka wa Uwahabi nchini Iraq vinakusudia kueneza fikra za Uwahabi na kuwashawishi waombolezaji wa Arbaini ya Imam Hussein (as) kutozuru maeneo matakatifu na makaburi ya Maimamu watoharifu, kuzusha shaka katika Ushia na kuwafanya Mashia watilie shaka itikadi zao.
Akifafanua suala hilo, Muhmoud as-Swafi, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Iraq amesema kuwa Mawahabi wamekuwa wakitawanya vitabu hivyo vya upotofu miongoni mwa wafuasi na wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume, Ahlul Bait (as) ambao hivi sasa wanafanya misafara mirefu ya kutembea kwa miguu kutoka miji mbalimbali ya Iraq kwenda kuomboleza Arbaini ya Imam Hussein huko katika mji mtakatifu wa Karbala, alikozikwa Imam Hussein (as) na kuwashawishi wasifanye ibada hiyo muhimu ya kidini.
Amesema katika vitabu hivyo vya upotofu kuna hadithi za uongo zinazonasibishwa kwa Mtume (saw) kwa ajili ya kuthibitisha madai yasiyo na msingi ya Mawahabi. As-Swafi amesema utumiwaji wa hadithi dhaifu na za uongo ni moja ya mbinu za kawaida zinazotumiwa na Mawahabi kwa ajili ya kuwapotosha wafauasi wa Ahlul Bait (as) na kujaribu kudhoofisha fikra imara za Watu wa Nyumba ya Mtume (saw).
Amesema kuwa Mawahabi ambao hawajafanikiwa kuwashawishi waombolezaji kugeuza mawazo yao kuhusiana na suala hilo wamekuwa wakilipiza kisasi kwa kutekeleza vitendo na mauaji ya kigaidi dhidi yao. 932580