Taarifa iliyotolewa na chama hicho imeitaka Mamlaka ya Ndani ya Palestina kujiondoa kwenye mazungumzo hayo haraka iwezekanavyo.
Sehemu moja ya taarifa hiyo imesema kuwa: "Mazungumzo hayo yanadhamini maslahi ya Marekani na utawala ghasibu wa Israel tu na kwa msingi huo Mamlaka ya Ndani ya Palestina inapaswa kujiondoa kwenye mazungumzo hayo haraka iwezekanavyo".
Chama cha Al Amal al Islami cha Jordan kimesema mazungumzo hayo ni njia ya kuiokoa Israel kwani harakati za wananchi katika nchi za Kiarabu zinahatarisha utawala huo ghasibu na viongozi wake sasa wanataka kopotosha fikra za waliowengi kwa kutumia mazungumzo hayo.
Chama hicho kimesema kufanya vikao na mazungumzo na utawala wa Kizayuni wa Israel kunatumiwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika kampeni za uchaguzi na kuwasababishia madhara wananchi wa Palestina.
Chama hicho ambacho kinafungamana na harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Jordan kumemalizia kwa kusema: Njia pekee ya kuikomboa Palestina ni kufanya mapatano ya kitaifa kati ya makundi yote ya mapambano ya ukombozi. 934364