Kwa mujibu wa gazeti la Nigeria Tribune, Kanali Victor Ebhaleme amesema kuwa wakuu wa kikosi hicho wamechunguza kwa makini madai hayo na kupata kuwa yalikuwa ya uongo na yasiyo na msingi wowote. Amesema madai hayo yametolewa na kundi la Boko Haram kwa madhumuni ya kuvuruga hatua kali ambazo zinachukuliwa dhidi yake na jeshi.
Kundi la kigaidi la Boko Haram linahesabiwa kuwa tawi la kundi la al-Qaida nchini Nigeria ambalo katika siku za hivi karibuni limekuwa likitekeleza vitendo vya kigaidi dhidi ya Wakristo na Waislamu wa nchi hiyo.
Kanali Ebhaleme amesema kwamba kwa kutilia maanani kuwa kikosi kilichotajwa kinaundwa na maafisa Wakristo na Waislamu na waliopewa mafunzo muhimu kuhusiana na jinsi ya kuheshimu matukufu ya wafuasi wa dini tofauti, ni jambo lililo mbali kwamba maafisa hao wamevunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani. 936514