Gazeti la al Ahram linalochapishwa nchini Misri limeandika kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya India alisema jana baada ya kukutana na mkuu wa jimbo la Rajasthan Ashok Gehlot kwamba safari ya Salman Rushdie nchini India imefutwa kutokana na maandamano yanayoendelea kufanywa na Waislamu kote nchini.
Watayarishaji wa Tamasha ya Fasihi Jaitapur mjini New Delhi wametangaza leo kwamba murtadi Salman Rushdie hatashiriki katika tamasha hiyo kutokana na kushadidi maandamano ya Waislamu katika mji wa New Delhi.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Darul Ulum ambacho kina ushawishi mkubwa nchini India ndicho kinachoongoza upinzani dhidi ya safari murtadi Salman Rushdie nchini humo.
Salman Rushdie raia wa Uingereza mwenye asili ya India mwaka 1988 alichapisha kitabu alichokiita Aya za Shetani ambacho kinadhalilisha na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu hususan Mtume Muhammad (saw). Kutokana na uhalifu huo mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Ruhullah Khomeini alitoa fatua akihalalisha damu ya mwandishi huyo na kuwataka Waislamu kote dunia kumuua murtadi huyo popote pale atakapokuwa. 937748