IQNA

Ayatullah Hamedani:

Niko tayari kufanya mdahalo na Mawahabi kwa msingi wa Qur'ani

17:07 - January 18, 2012
Habari ID: 2259484
Ayatullah Nouri Hamedani ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa nchini Iran amesema kuwa Uwahabi ni balaa kwa Waislamu wote na kusisitiza kuwa yuko tayari kufanya mdahalo na Mawahabi kwa kutegemea vitabu vyao wenyewe na kwa msingi wa Qur'ani na Hadithi.
Hata hivyo Ayatullah Hamedani amesisitiza kuwa Mawahabi si watu wa mantiki na mazungumzo.
Ayatullah Hamedani amesema hayo leo katika hadhara ya watayarishaji wa mkutano wa Hadhrat Zainab (as) katika mji mtakatifu wa Qum na kuongeza kuwa Mawahabi wanaudhulumu Uislamu kwa kutumia fedha za Saudi Arabia na Qatar na wanashirikiana na kutumikia Marekani na Wazayuni.
Mwanazuoni huyo mkubwa wa Kiislamu amesisitiza kuwa Uwahabi ni balaa kubwa kwa Waislamu na kwamba mikutano kama huu wa Hadhrat Zainab (as), inapaswa kuweka wazi hatari ya fikra za Kiwahabi.
Amesema mchango uliotolewa na Bibi Zainab binti Ali bin Abi Twalib (as) katika medani ya Karbala haujaarifishwa ipasavyo. Ameongeza kuwa katika kipindi cha sasa ambako mwamko wa Kiislamu umeenea kote dunia kuna udharura wa kumtangaza Bibi Zainab kama kinara wa mwamko katika historia ya Kiislamu. 937792

captcha