IQNA

Mamilioni ya Waislamu washiriki katika maombolezo ya kifo cha Mtume Mtukufu (saw), Najaf

14:20 - January 22, 2012
Habari ID: 2260904
Mamilioni ya Waislamu kutoka maeneo mbalimbali duniani wameshiriki katika shughuli za maombolezo ya kukumbuka siku ya kufariki dunia Mtume Muhammad (saw) katika mji mtakatifu wa Najaf, mahala palipo na kaburi la ndugu na khalifa wake, Imam Ali bin Abi Twalib (as).
Ripoti zinasema kuwa Waislamu zaidi ya milioni mbili wameshiriki katika maombolezo hayo na kukumbuka tukio chungu la kuaga dunia rehma ya walimwengu na Mtume wa Nuru Muhammad bin Abdullah (saw).
Kamati ya Usalama ya Baraza la mji mtakatifu wa Najaf imetangaza kuwa maelfu ya Waislamu kutoka maeneo mbalimbaki duniani wameshiriki katika shughuli hiyo ya mamombolezo ya kukumbuka kifo cha Mtukufu Mtume Muhammad (saw).
Kamati ya Usalama ya Baraza la mji wa Najaf imetangaza kuwa zaidi ya watu laki moja kutoka nchi za nje waliwasili mjini humo kwa ajili ya kushiriki kwenye shughuli ya mamombolezo ya kifo cha Mtume (saw) na kwamba baraza hilo limetayarisha mazingira bora ya wafanyaziara hao.
Mkuu wa Kamati ya Usalama ya Baraza la mji wa Najaf Luayy al Yasiri amesema kuwa makundi ya wafanyaziara kutoka nchi za nje yaliwasili mjini Najaf kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji huo na wengine kupitia mipaka ya nchi kavu.
Al Yasiri amesema kuwa mazuwari hao ni kutoka nchi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Lebanon, nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi, Marekani na nchi mbalimbali za Ulaya.
Hatua makhsusi za kiusalama zimechukuliwa na kikosi cha usalama cha mji mtakatifu wa Najaf kwa ajili ya kudhamini usalama wa wafanyaziara hao.
Tarehe 28 Safari kila mwaka ambayo inakumbusha tukio chungu la kufariki dunia mbora wa viumbe Mtume Muhammad (saw), maelfu ya Waislamu kutoka ndani na nje ya Iraq huelekea katika mji mtakatifu wa Najaf na kushiriki kwenye shughuli ya kukumbuka kifo hicho katika Haram ya wasii na khalifa wake, Imam Ali bin Abi Twalib (as). 938652
captcha