IQNA

Harakati za Waislamu wa Algeria za kushinda uchaguzi ujao wa bunge

12:28 - January 31, 2012
Habari ID: 2265511
Abdallah Jaballah, kiongozi wa chama cha Uadilifu na Maendeleo cha Algeria ametabiri kwamba vyama vya Kiislamu vitashinda uchaguzi ujo wa bunge la nchi hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya atlasinfo, Jaballlah amesema kuwa vyama vya Kiislamu vina matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi huo. Amesema matumaini hayo hayatokani na ushindi wa harakati za Kiislamu katika nchi za Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika bali ni kutokana na histori ndefu ya wananchi wa Algeria katika kutetea na kupigania Uislamu.
Jaballah amesema anafahamu vyema matokeo ya chaguzi zilizofanyika Algeria katika miaka ya 1991, 1997 na 1999 na kwamba kwa msingi huo ana matumaini makubwa ya vyama vya Kiislamu kushinda uchaguzi ujao wa bunge. Amesisitiza kwamba kwa kutilia maanani ukweli kuwa wananchi wa Algeria ni Waislamu, hilo tu linatosha kwao kuwachagua wawakilishi ambao ni Waislamu.
Tunakumbusha hapa kwamba Sheikh Abdallah Jaballah ambaye huko nyuma aliasisi vyama viwili vya Kiislamu vya an-Nahdha na Islah alijiondoa katika vyama hivyo hivi karibuni kutokana na hitilafu za ndani na kuamua kuunda chama kipya cha Kiislamu cha Uadilifu na Maendeleo miezi michache iliyopita. 943995
captcha