IQNA

ISESCO kuzungumzia mkondo wa ukurubishaji wa madhehebu ya Kiislamu katika kikao cha Umoja wa Kiislamu Tehran

16:11 - February 08, 2012
Habari ID: 2271135
Hotuba ya Katibu Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni wa Kisilamu la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO, kuhusiana na mwenendo wa ukurubishaji pamoja wa madhehebu ya Kiislamu inatazamiwa kusomwa katika kikao cha kimataifa cha Umoja wa Kiislamu kinachoendelea mjini Tehran.
Hotuba hiyo itasomwa na mwakilishi wa katibu mkuu huyo katika kikao hicho.
Katika kikao cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kilichofanyika nchini Malaysia mwaka 2003, shirika la ISESCO lilitangaza siasa za kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu kuwa mojawapo ya malengo yake muhimu na kubuni kamati kuu ya kushughulikia suala hilo.
Kikao cha Kimataifa cha 25 cha Wiki ya Umoja wa Kiislamu kimeanza leo Jumatano tarehe 8 Februari mjini Tehran ambapo wanachama 271 wa Baraza Kuu la Taasisi ya Ukurubishaji wa Madhehebu ya Kiislamu na shakhsia mbalimbali wa kielimu na kiutamaduni kutoka nchi 50 wanashiriki. Kikao hicho kitaendelea kwa muda wa siku tatu. 949947
captcha