IQNA

Rais Ahmadinejad: Madola ya kibeberu yanataka kuunusuru utawala wa Kizayuni

21:35 - February 08, 2012
Habari ID: 2271528
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema madola ya kibeberu na istikbari yanatumia vyombo vya habari na kiasi kikubwa cha fedha kutawala eneo la Mashariki ya Kati na kuunusuru utawala haramu wa Israel.
Rais Ahmadinejad ameyasema hayo alipohutubu kikao cha ufunguzi wa Kongamano la 25 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu mjini Tehran.
Kwenye hotuba hiyo ya ufunguzi, Rais Ahmadinejad ametoa wito wa kudumishwa na kuimarishwa zaidi umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu. Ameongeza kuwa ni kupitia Umoja ambapo Waislamu wataweza kukabiliana na njama za kila leo za maadui wa Uislamu. Ameongeza kuwa Marekani na utawala haramu wa Israel zinaongoza katika orodha ya maadui wa Uislamu na Waislamu.
Lengo la kongamano hilo ni kuandaa uwanja wa kuwepo umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu ili kuwawezesha wasomi na wanazuoni wake kukurubisha pamoja mitazamo yao ya kifikra na kielimu katika nyanja mbalimbali za taaluma za Kiislamu.
Kongamano hilo linahudhuriwa na washiriki 271 kutoka nchi 50 duniani.
950173
captcha