IQNA

Pakistan yaandaa Maonyesho ya Kimataifa ya Chakula Halali

16:05 - February 13, 2012
Habari ID: 2273371
Maonyesho ya Kimataifa ya Chakula Halali Barani Asia yanatazamiwa kufanyika katika mji wa Karachi nchini Pakistan.
Kwa mujibu wa tovuti ya ecocci.com maonyesho hayo yatafanyika kuanzia Aprili 17-19 mwaka huu katika Kituo cha Maonyesho mjini Karachi.
Kumekuwa na ongezeko la utumizi wa bidhaa za vyakula halali kote duniani katika kipindi cha miaka kadhaa sasa na mkondo huo unazidi kuongezeka na kuvutia mashirika ya Ulaya yanayotaka kuuza bidhaa katika nchi za Kiislamu.
Inakadiriwa kuwa thamani ya soko la vyakula halali duniani sasa ni takribani $ billion 632 kila mwaka. Hiyo ni takribani asilimia 16 ya soko lote la kimataifa. Kustawi soko la vyakula halali kumezidisha haja ya kudhibiti soko la bidhaa halali ili kuhakikisha kuwa chakula halali kinachouzwa ni halali kweli kama inavyotangazwa.
Maonyesho hayo ya Karachi yatawakutanisha wafanyabiashara, wawekezaji na wanunuzi kutoka maeneo yote ya dunia.
952420
captcha