Mkutano huo umefanyika chini ya usimamizi wa Sheikh wa al Azhar Ahmad Tayyib kwa lengo la kuvunja mzingiro wa Wazayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na kuitetea Quds Tukufu.
Mkutano huo unahuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Kiislamu na Kikristo na maaafisa wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na inatazamiwa kuwa kutatolewa taarifa ya mwisho baadaye hii leo.
Pamoja na mambo mengine mkutano huo wa kimataifa unachunguza hali ya sasa ya mji mtakatifu wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala za Kizayuni wa Israel.
Washiriki wanajadili na kubalidilishana mawazo kuhusu siasa za utawala vamizi wa Israel za kukata njia za mawasiliano za mji wa Quds na ratiba za kivitendo za kuunga mkono mwamko na harakati za wakazi wa mji huo za kukabiliana na siasa za kibaguzi za Israel. 953855