IQNA

Wanazuoni wataka kupigwa marufuku uvunjiwaji heshima nembo za Ushia nchini Kuwait

12:29 - February 16, 2012
Habari ID: 2275187
Kwa kuzingatia ongezeko la vitendo vya dharau na kuvunjiwa heshima itikadi na nembo za Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Kuwait, wanazuoni 32 wa Kishia wa nchi hiyo wametoa taarifa wakiwataka watawala wa Kuwait wapige marufuku dharau dhidi ya itikadi za Mashia nchini humo.
Wamelaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Imam wao wa 12 Imam Mahdi (af) na kusema kuwa jambo hilo ni katika mfululizo wa hujuma ya kuvunjia heshima madhehebu ya Watu wa Nyumba ya Mtume (saw), itikadi na matukufu ya Mashia.
Wanazuoni wa Kishia wa Kuwait wamesisitiza kuwa jambo hilo haliwezi kuvumiliwa katika mazingira nyeti na tata ya hivi sasa katika Mashariki ya Kati. Wamewataka Waislamu kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu, kutetea thamani na matukufu ya Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) na kuheshimu imani za watu wengine.
Vilevile wametahadharisha kuwa dharau dhidi ya itikadi za kidini ina hatari ya kuzusha fitina katika jamii ya nchi hiyo. Wamewataka watawala wa Kuwait kutekeleza majukumu yao ipaswavyo kwa kutozembea katika kutekeleza sheria dhidi ya watu wanaovunjia heshima matukufu ya kidini. Wanazuoni hao wamewataka pia viongozi wa serikali ya Kuwait watekeleze sheria kwa usawa bila kubagua baina ya raia wa nchi hiyo. Wamesema kubaguliwa baadhi ya watu wa nchi hiyo kutapunguza imani ya wananchi kwa viongozi wa nchi hiyo, jambo ambalo bila shaka litakuwa na matokea mabaya kwa nchi hiyo. 954082
captcha