Taarifa hiyo inasema kuwa maadui wa Kizayuni wameendelea kutekeleza jinai zao zikiwemo za kuyahudisha Quds, kukanyaga matukufu na kuharibu nyumba na maeneo matukufu ya Wapalestina pamoja na kupora zaidi ardhi zao.
Hizbullah imesisitiza kwamba utawala haramu wa Israel ndio unaowachochea walowezi wa Kizayuni kushambulia Msikiti wa al-Aqsa na maeneo mengine matakatifu ya Waislamu na Wakristo. Imesema utawala ghasibu wa Tel Aviv umekuwa ukitumia vibaya matukio ya kisiasa yanayoendelea sasa katika nchi za Kiarabu za Mashariki ya Kati kwa kueneza siasa zake za kuyahudisha Quds Tukufu na kukanyaga matukufu mengine ya Waislamu na Wakristo wa Palestina kwa kutambua kuwa mataifa ya eneo hili muhimu yameshughulishwa na matukio hayo.
Hizbullah imewataka Waislamu na Wakristo kote ulimwengu kusimama na kufanya maandamano ya kutetea Quds Tukufu kwa sababu wananchi wa Palestina wanafahamu vyema kwamba watawala wengi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu ambao ni vibaraka wa nchi za Magharibi, hawatachukua hatua yoyote muhimu ya kupinga jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya matukufu ya Kiislamu na Kikristo.
Imesema kwa kunyamazia kimya jinai hizo, Umoja wa Mataifa unashirikiana moja kwa moja na utawala huo katika kutekeleza jinai zake dhidi ya Wapalestina na ulimwengu mzima wa Kiislamu. 957424