IQNA

Wanachama wa Hizbullah wakutana na Mufti Mkuu wa Lebanon

16:08 - February 21, 2012
Habari ID: 2278091
Wajumbe kadhaa wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon wamekutana na Mufti Mkuu wa nchi hiyo Sheikh Mohammad Rashid Kabbani.
Kwa mujibu wa tovuti ya loreintlejour, mkutano huo umefanyika Februari 20 ambapo ujumbe wa wabunge wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu yaani Hizbullah wakiongozwa na Abdulmajid Ammar, mwanachama wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah' ulikutana na Mufti Kabbani na kujadili masuala ya kieneo na kimataifa.
Ammar amesema kuwa katika mkutano huo pande mbili zilisisitiza umuhimu wa umoja wa watu wa Lebanon, wakiwemo Mashia , Masuni na Wakristo. Wamesema umoja wa kitaifa ndio njia pekee ya kuzuia hitilafu.
Ameongeza kuwa, wote walioshiriki katika mkutano huo walibainisha wazi kuwa kuna udharura wa kuhimiza uthabiti Lebanon. Amesisitiza kuwa Hizbullah, kama mwakilishi wa Mashia Lebanon, iko tayari kufanya mazungumzo na makundi yote ya kisiasa nchini humo kwa lengo la kuimarisha umoja wa kitaifa.
957492
captcha