Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema kitendo cha wanajeshi wa Marekani cha kuivunjia heshima Qur'ani kilikuwa cha makusudi na kilichotokana na chuki yao dhidi ya Uislamu.
Kwingineko katika hotuba yake, khatibu wa Sala ya Ijumaa ameishukuru serikali ya Iran kwa kukata uuzaji mafuta ya petroli kwa nchi kadhaa za Ulaya. Huku akiaashiria kuongezeka bei ya mafuta katika masoko ya dunia na kuibuka mgogoro wa kiuchumi katika nchi za Ulaya, Ayatullah Khatami amewanasihi viongozi wa Ulaya waache kufuata kibubusa sera za kijitanua za Marekani ili wasikumbwe na matatizo.
Kwingineko katika hotuba yake khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema kuwa kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi ujao wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (bunge) ni wajibu wa kiakili na kisheria. Ayatullah Khatami ameongeza kuwa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu inaongoza masuala ya nchi na ni nembo ya demokrasia ya Kiislamu.
Akihutubia halaiki kubwa ya waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Khatami ameongeza kuwa kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi ujao ni jambo ambalo litaimarisha Uislamu na mfumo wa Kiislamu Iran.Ayatullah Khatami amesema maadui wanataka kudunisha uchaguzi ujao. Amelinasihi taifa kubwa la Iran kuchagua bunge linaloenda kwa msingi wa mfumo mtakatifu wa Kiislamu kwa kuwapigia kura watu wanaofaa na wenye umahiri wa kisiasa walio mashujaa, wenye uwezo katika kutekeleza majukumu, wenye kufuata sheria na wenye kumtii faqihi mtawala.
Khatibu wa Muda wa Sala ya Ijumaa Tehran vile vile ametoa wito kwa wanaogombea viti katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran wanapaswa kuzingatia maadili ya uchaguzi na wasiwachafulie jina wapinzani wao au wanaowaunga mkono. Uchaguzi ujao wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran utafanyika Ijumaa ijayo tarehe pili Machi. Kampeni za uchaguzi zilianza jana Alkhamisi na zitaendelea hadi machi mosi.
959265