IQNA

ISESCO yalaani Wamarekani kwa kuchoma moto Qur'ani Afghanistan

12:54 - February 25, 2012
Habari ID: 2279725
Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni (ISESCO) limelaani vikali kitendo cha wanajeshi wa Marekani kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu katika kituo cha kijeshi cha Marekani cha Bagram nchini Afghanistan.
Taarifa ya ISESCO imesema hatua ya wanajeshi vamizi wa Marekani kuchoma moto nakala za Qur'ani katika nchi mwanachama wa ISESCO ni kitendo cha kishenzi na kibaguzi. ISESCO imesema vikosi vya Marekani na NATO vinavyokalia mabavu Afghanistan vinabeba lawama zote za kitendo hicho cha kishenzi.
ISESCO pia imetoa wito kwa nchi wanachama, jamii ya kimataifa, Umoja wa Mataifa na taasisi zingine za kimataifa kulaani vikali jinai hiyo na kutoa mashinikizo ili wahusika waadhibiwe kisheria.
ISESCO imesema kitendo hicho ni hujuma ya moja kwa moja dhidi ya Waislamu duniani na ni sawa na jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. ISESCO imesema kutowaadhibi wanajeshi wa Marekani walioteketeza Qur'ani Afghanistan ni sawa na kuidhinisha vitendo vyao.
959302
captcha