Waandamanaji waliokusanyika mjini Lahore walitangaza upinzani na hasira zao kubwa dhidi ya kitendo cha askari wa Marekani cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu katika kituo cha anga cha Bagram nchini Afghanistan.
Maandamano kama hayo yaliyosimamiwa na chama cha Jamaat Islamiyya na Jamaat Daawah vya Pakistan yalifanyika pia katika miji mingine ya nchi hiyo ambapo washiriki walitoa wito wa kuchukuliwa hatua kali watu waliotekeleza kitendo hicho kiovu.
Waandamanaji katika mji wa Peshawar walichoma moto bendera za Marekani na kutoa wito wa kufukuzwa askari wa Marekani nchini Afghanistan.
Mjini Islamabad, waandamanaji walitoa taarifa iliyozitaka nchi za Kiislamu kutazama upya uhusiano wao na Marekani na kwamba zisiruhusu matukufu ya Kiislamu kuvunjiwa heshima.
Maandamano kama hayo ya kulaani kitendo kiovu cha askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani yalifanyika jana katika miji mbalimbali ya Pakistan baada ya swala za Ijumaa. 959503