Taarifa ilioyotolewa na jumuiya hiyo imesema kuwa askari wa Marekani wameendelea kuvunjia heshima matukufu ya Waislamu katika nchi za Kiislamu na vitendo kama hivyo vimekwishafanyika huko nyuma huko Afghanistan na Marekani.
Taarifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Maulama Waislamu imeeleza wasiwasi wake kuhusu vitendo hivyo viovu vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Afghanistan na kusema uhalifu huo unachochea hisia za Waislamu kote duniani.
Jumuiya hiyo imesisitiza kuwa kitendo cha askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu ni hatua ya kichochezi na ya kuaibisha ambayo inazidisha uhasama na chuki kati ya mataifa mbalimbali na kusababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia nchini Afghanistan.
Jumuiya hiyo imewataka Waislamu kote duniani kukabiliana na hatua kama hizo sambamba na kuheshimu maadili ya Kiislamu. 961525