IQNA

Kamati ya Kiislamu na Kikristo yatoa wito wa kulindwa Msikiti wa al Aqsa

12:01 - February 28, 2012
Habari ID: 2281984
Kamati ya Kiislamu na Kikristo ya Kulinda Quds Tukufu imezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za kuulinda Msikiti wa al Aqsa mbele ya mashambulizi yanayoongezeka kila siku ya utawala ghasibu wa Israel.
Taarifa ya kamati hiyo iliyosomwa katika mkutano wa kimataifa wa kutetea Quds unaofanyika Qatar imewataka viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za kusimamisha mashambulizi ya Utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa al Aqsa hususan mashambulizi yanayofanywa na Walowezi wa Kiyahudi wenye misimamo mikali.
Katibu Mkuu wa mkutano huo Hana Issa amesema mashambulizi yanayofanywa na walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na njama zao za kutaka kudhibiti msikiti huo na kuchimba mashimo chini yake vinapaswa kukomeshwa haraka iwezekanavyo.
Amesema walowezi wa Kizayuni wameuzingira Msikiti wa Quds kwa kuweka vituo kadhaa vya upekuzi kandokando yake na amewataka washiriki katika mkutano huo wa kimataifa kuitetea Quds Tukufu. 961574

captcha