IQNA

Wananchi wa Yemen wafanya maandamano kulalamikia uchomaji moto Qur'ani Afghanistan

15:22 - February 29, 2012
Habari ID: 2283075
Wananchi wa Yemen wamefanya maandamano makubwa nchini humo kulaani kitendo cha askari jeshi wa Marekani walioko nchini Afghanistan cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu.
Maandamano hayo yaliyoanzia katika eneo la Masik yalimalizikia mbele ya ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.
Waandamanaji walipiga nara za kulaani vikali kitendo cha askari hao cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa kuichoma moto katika kituo chao cha kijeshi huko Bagram nchini Afghanistan. Waandamanji hao waliochoma moto bendera ya Marekani kutokana na hasira waliyokuwa nayo pia walitaka kususiwa bidhaa zote za Marekani nchini humo na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria wahusika wa kitendo hicho cha jinai dhidi ya Waislamu.
Siku ya Jumatatu pia kundi kubwa la raia wa Yemen lilifanya maandamano mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Sanaa na kulaani vikali kitendo cha askari wa nchi hiyo cha kuchoma moto Qur'ani.
Tunakumbusha hapa kwamba kitendo hicho cha kipumbavu cha askari wa Marekani nchini Afghanistan kimeamsha hasira kubwa ya wananchi wa nchi hiyo dhidi ya Marekani. Maandano kama hayo pia yamefanyika katika pembe tofauti za dunia. 962631
captcha