Sheikh Muhammad Hussein, Khatibu wa Masjidul Aqsa amesema kuwa, amewataka Waislamu kote ulimwenguni kuuhami msikiti huo mtakatifu na kibla cha kwanza cha Waislamu unaoandamwa na njama za maadui Wazayuni.
Aidha amewataka Waislamu kwenda kufanya ibada zao katika msikiti huo na amepinga vikali fatuwa zinazowazuia wasiokuwa Wapalestina kutembelea Quds.
Sheikh Muhammad Hussein ameashiria nafasi ya Misri katika kuihami Quds na Msikiti wa al-Aqswa na kusisitiza kwamba, hatua zozote zile dhidi ya msikiti huo mtakatifu zitahatarisha usalama wa taifa wa Misri.
Wakati huo huo, Mufti wa Quds na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina amezitaka Hamas na Fat'h kuhitimisha hitilafu zao za ndani na badala yake kudumisha umoja na mshikamano.
969063