IQNA

Mufti wa Quds aonya juu ya kuharibiwa Masjidul Aqsa kupitia mtetemeko bandia wa ardhi

14:58 - March 11, 2012
Habari ID: 2289682
Mufti wa Quds ameonya juu ya hatua ya utawala wa kibaguzi wa Israel ya kutumia mtetemeko bandia wa ardhi katika kuharibu Masjidul Aqsa.
Gazeti la al-Ittihad linalochapishwa Imarati limeandika kuwa Mufti Sheikh Muhammad Hussein amezitaka nchi za Kiislamu na Kiarabu kuchukua hatua za dharura kwa lengo la kuuzuia utawala haramu wa Israel kufanya mtetemeko huo chini ya msikiti huo mtakatifu.
Ameitaka Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la umoja huo UNESCO na kulifahamisha athari mbaya za uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kutaka kubomoa msikiti huo kwa njia ya mtetemeko bandia wa ardhi. Amesema wakazi wa Quds wamekuwa wakitekeleza hatua tofauti za kuulinda msikiti huo dhidi ya hujuma hiyo ya Wazayuni, ikiwa ni pamoja na kukusanyika kwa wingi katika msikiti huo kwa lengo la kutekeleza ibada.
Sheikh Muhammad Hussein amesema vyombo vya habari pia vinapasa kuwa na mchango katika kuzuia kuharibiwa msikiti huo kwa kuakisi na kufichua njama za utawala wa Tel Aviv za kuanzisha mtetemeko huo bandia, kuchimba njia za chini kwa chini zinazodhoofisha nguzo za msikiti huo na hujuma ya mara kwa mara inayotekelezwa na utawala huo katika msikiti huo. 969063
captcha