IQNA

Ujenzi wa msikiti mkubwa zaidi barani Ulaya waanza Ujerumani

13:38 - March 12, 2012
Habari ID: 2290132
Ujenzi wa msikiti mkubwa zaidi barani Ulaya umeanza huko katika mji wa Cologne nchini Ujerumani kwa ushirikiano wa shirika moja kubwa la Uturuki.
Kwa mujibu wa gazeti la Yaum as-Sabe' linalochapishwa Misri, moja ya mashirika makubwa zaidi ya Uturuki nchini Ujerumani limepewa jukumu la kujenga msikiti huo ambao utakuwa mkubwa zaidi nchini humo na katika bara zima la Ulaya.
Msikiti huo ambao utagharimu Euro milioni 34 utakuwa wa 1000 kujengwa barani Ulaya. Mkuu wa Baraza la Kiidara la msikiti huo amesema kuhusiana na suala hilo kwamba msikiti huo utakuwa na uwezo wa kubeba waumini 2000 na kutoa huduma muhimu kwa Waislamu wa nchi hiyo ambao wanakisiwa kuwa milioni 4.
Akizungumzia suala hilo, Jurgen Roters, meya wa mji wa Cologne amesema kwamba ujenzi wa msikiti huo utauletea mji huo umashuhuri wa kimataifa. Amesema ujenzi wa msikiti huo utakamilika mwakani na kufunguliwa kwa ajili ya Waislamu kutekelezea humo ibada zao. 969999
captcha