IQNA

Kijana wa Tunisia aliyemvunjia heshima Mtume (saw) akamatwa

16:49 - March 13, 2012
Habari ID: 2291209
Maafisa wa mahakama katika eneo la al-Mahdiyya nchini Tunisia wamemtia nguvuni kijana mmoja aliyemvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw).
Kwa mujibu wa televisheni ya al-Manar ya nchini Lebanon, kundi moja la wataalamu wa Tunisia lilipewa jukumu la kufuatilia na kufanya uchunguzi kuhusiana na kitendo hicho kilichofanywa na kijana huyo wa Tunisia kupitia mtandao wa Facebook na kufanikiwa kumtambua na kisha kumuarifisha kwa vyombo husika vya polisi ambavyo vilimtia nguvuni na kumkabidhi kwa vyombo vya mahakama.
Kwa mujibu wa ripoti zilizotufikia, kijana huyo aliweka picha za dharau na kejeli dhidi ya Mtume Muhammad (saw) katika ukurasa wake wa facebook na kisha kuandika maneno ya kumvunjia heshima Mtume (saw) chini ya picha hizo. 970845
captcha