IQNA

Spika wa Bunge la Iran atoa wito wa Umoja miongoni mwa Waislamu

11:33 - March 20, 2012
Habari ID: 2293906
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran amesema, kuna udharura wa kuwepo ushirikiano miongoni mwa Waislamu duniani ili waweze kufikia malengo matakatifu ya Uislamu.
Katika ujumbe wake kwa maspika wa mabunge ya nchi za Kiislamu kwa mnasaba wa sikukuu ya Nowruz, Ali Larijani ameelezea matumaini yake kuwa, mataifa yote ya Waislamu yatakutanika pamoja chini ya kivuli cha Qur'ani Tukufu. Ameongeza kuwa, kwa kufuata mafundisho ya Qur'ani, Waislamu wataweza kupata mshikamano na umoja baina yao.
Sambamba na ujumbe wake huo, Spika wa Majlisi ya Kiislamu ya Iran pia amewatunuku maspika wa mabunge ya Kiislamu duniani zawadi ya kopi ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa mkono, miaka 1000 iliyopita hapa Iran kwa kutumia hati za Kufi.


973997
captcha