Kwa mujibu wa Televisheni ya Press, Bi Amina Baghajati mwanamke wa Kiaustria aliyesilimu hivi karibuni anasema, wananchi wa nchi hiyo wana shauku ya masuala ya kiroho na wanahisi kwamba, wana hali fulani ya mapungufu katika maisha yao ya kila siku.
Utafiti uliofanywa unaonesha kwamba, akthari ya Wakristo wa Austria ambao ni waumini wa madhehebu ya Kikatoliki wamepoteza imani na dini yao hasa kutokana na kashfa za makasisi wa Kanisa Katoliki za kuwabaka na kuwanajisi watoto wadogo. Wakristo hao wamekuwa wakisilimu kwa kasi wakiamini kwamba, Uislamu ndilo kimbilio na mwokozi wao pekee.
Austria ina zaidi ya wakazi milioni 8 na katika kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita zaidi ya Wakristo 500 wamesilimu na kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu.
Pamoja na kuwepo chuki dhidi ya Uislamu huko Ulaya na Marekani, idadi kubwa ya watu barani humo wanazidi kusilimu wakiwemo watu kutoka familia mashuhuri.
Hivi karibuni Sean Stone, mwana wa mtengeneza filamu mashuhuri wa Marekani Oliver Stone alisilimu akiwa Iran na kubadilisha jina lake kuwa Ali. Aidha Lauren Booth, dada wa Cherie Blair mke wa Tony Blair Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza alisilimu akiwa Iran mara baada ya kuzuru Haram ya Bibi Fatimat Maasumah Alayha Salaam katika mji wa Qum.
984777