IQNA

Vyombo vya habari Korea Kusini vyapotosha sura ya Uislamu

18:55 - April 14, 2012
Habari ID: 2304553
Vyombo vya habari na vya mawasiliano ya umma nchini Korea vinalaumiwa kwa kuonesha sura isiyokuwa sahihi kuhusu Uislamu.
Tovuti ya On Islam imemnukuu Shariq Said, Muislamu mwenye asili ya Pakistan anayeishi nchini Korea Kusini akisema kuwa licha ya kwamba Waislamu wanaishi kwa amani na upendo kamili nchini humo lakini vyombo vya habari vimekuwa vionesha sura isiyokuwa sahihi kuhusu Uislamu.
Waislamu wa mji mkuu wa Korea, Seol hukusanyika kila siku ya Ijumaa katika msikiti pekee wa Waislamu mjini humo na kutekeleza ibada ya Swala ya Ijumaa. Aghlabu ya Waislamu hao ni kutoka nchi za Mashariki ya Kati, kusini na kusini mashariki mwa Asia na wanaishi katika maeneo ya kandokando ya msikiti huo.
Muhdi Fakhal, mwanafunzi wa chuo kikuu kutoka Malaysia anayesoma nchini Korea Kusini anasema, Waislamu wanadhihirishwa katika vyombo vya habari vya nchi hiyo kuwa ni watu maskini hohehahe ambao daima huwa katika hali ya ogomvi na mivutano, suala ambalo amasema, halina ukweli wowote.
Amesema kuwa Waislamu nchini Korea Kusini wanakabiliwa na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na uhaba wa misikiti na maeneo ya ibaya.
Muislamu Mkore Kusini Jun Song Ju ambaye alisimu na kukubali dini tukufu ya Uislamu akiwa Ireland anasema kuwa, suala la kupata chakula halali ni miongoni mwa matatizo makubwa yanayowasumbua Waislamu nchini Korea Kusini. 985382


captcha