IQNA

Mbunge wa Israel akosoa siasa za kibaguzi za utawala huo

21:21 - April 17, 2012
Habari ID: 2307102
Mbunge Mwarabu wa Israel Ahmad al Tibi amekosoa vikali siasa za kibaguzi za utawala huo haramu dhidi ya wananchi wanaokandamizwa wa Palestina.
Al Tibi ameiambia televisheni ya Press kwamba mwaka 1948 Waarabu walikuwa wakimilika asilimia 85 ya ardhi zao lakini hii leo wanamiliki asilimia 3 tatu ya ardhi hizo, suala ambalo linaakisi vyema kila kitu ikiwa ni pamoja na jinsi walivyofukuzwa katika ardhi za mababu zao, kughusubiwa mali na kufanywa wakimbizi.
Mbunge huyo wa Israel ameyasema hayo katika kikao cha Kanali ya Mfungamano wa Daima wa Ottawa na Palestina kilichofanyika nchini Canada.
Vilevile amelaani hatua ya Israel ya kuwazuia Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi na Ghaza kuingia katika Quds Tukufu na akasema kuwa utawala wa Israel uliiteka Quds Mashariki mwaka 1967 na tangu wakati huo umekuwa ukijenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika eneo hilo la Palestina. 987708
captcha