Mjumbe wa Kamati Kuu ya Kituo cha Habari cha Kiislamu cha Toronto Muhammad Abdullah amesema kuwa kwa mujibu wa mkataba uliotiwa saini na Kamisheni ya Usafirishaji ya Toronto, mabango na maandishi yanayowalingania Wacanada dini tukufu ya Kiislamu yatatundikwa katika vituo vinne vya metro (treni ya chini ya ardhi) kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Mabango na maandishi hayo yanawaelekeza wasomaji wake kwenye tovuti ya Ujue Uislamu ambayo inalingania Uislamu kwa lugha 85.
Wakati huo huo afisa mmoja wa Kamisheni ya Usafirishaji ya Toronto amejibu malalamiko yaliyowasilishwa na makundi yanayoupiga vita Uislamu dhidi ya hatua hiyo akisema kuwa sheria za Canada zinaruhusu matangazo kama hayo ya kidini. 988695