IQNA

'Uwezo mkubwa wa Iran ni kwa faida ya nchi za Kiislamu'

14:48 - April 21, 2012
Habari ID: 2309185
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, kuwa na nguvu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kwa manufaa ya nchi za Kiislamu na ni kwa ajili ya kuzitumikia nchi hizo hasa za eneo hili la Ghuba ya Uajemi.
Ayatullah Jannati amekosoa hatua za hivi karibuni za baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi dhidi ya Iran na kusema kuwa, nchi hizo hazipaswi kufuata misimamo yenye kuiletea manufaa Marekani na utawala haramu wa Kizayuni katika eneo hili, kwani kuwa na nguvu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kwa manufaa ya nchi za eneo hili.
Amesisitiza kuwa Marekani na washirika wake hawawezi kukabiliana na mawimbi ya mwamko wa Kiislamu yanaoendelea kushuhudiwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba, mwisho wa mabeberu hao umewadia.
Akiashiria duru mpya ya mazungumzo baina ya Iran na kundi la 5 + 1 yaliyofanyika mjini Istambul Uturuki Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema, mazungumzo hayo yalikuwa yenye manufaa hasa kwa vile nchi za Magharibi zimekubali kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina haki ya kustafidi na nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani.
989653
captcha