Israel imekuwa ikisambaza chakula cha aina hiyo katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
Habari hiyo imetangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afya ya Russia Gennady Onishchenko ambaye ameongeza kuwa Remedia ni aina ya chakula cha watoto wadogo kinachotengenezwa Israel na kimesambazwa nchini Russia. Amesisitiza kuwa chakula hicho kina madhara makubwa kwa afya ya watoto.
Ripoti zinasema kuwa baada ya kutolewa habari hiyo chakula hicho kimekusanywa na kuondolewa katika maduka yote ya Russia.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Moscow inapinga siasa za nchi za Magharibi na utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kadhia ya Syria na inasisitiza juu ya kutatuliwa mgogoro wa nchi hiyo kwa njia za amani. Vilevile Russia na China zimetumia kura ya veto dhidi ya azimio lililokuwa limependekezwa na Marekani na nchi za Magharibi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Syria, suala ambalo limeukasirisha mno utawala wa Kizayuni wa Israel. 990360