Munir al Barsh amesema kuwa hospitali za Ghaza zina uhaba wa zana za kitiba na aina 186 za madawa ambayo yameadimika katika maghala na maduka ya dawa, suala ambalo limezusha maafa makubwa kwa hospitali za watoto na vitengo vya upasuaji.
Al Barsh pia ameikosoa serikali ya ndani ya Palestina kwa kushirikiana na utawala ghasibu wa Israel katika kulizingira eneo la Ghaza na kutotuma hisa ya dawa na wakazi wa eneo hilo.
Ameitahadharisha jamii ya kimataifa kuhusu uwezekano wa kutokea maafa katika Ukanda wa Ghaza na amezitaja jumuiya zinazohusiana na madawa za shirika la Msalaba Mwekundu kuchuku hatua za kuwaokoa watu wa Ghaza kuhusu hali hiyo.
Mbali na uhaba mkubwa wa dawa na zana za kitiba, watu wanaodhulumiwa wa Ghaza wanasumbuliwa pia na ukosefu wa nishati kutokana na Misri kusimamisha utumaji wa gesi kwa wakazi wa eneo hilo.
Katika wiki za hivi karibuni Misri ilisimamisha kutuma nishati huko Ghaza na sasa wananchi wa eneo hilo hawana njia nyingine ya kudhamini nishati isipokuwa kutoka Israel nayo kwa bei kubwa kupita kiasi. 993275