Kwa mujibu wa televisheni ya CNN, at-Tamimi alisema kuwa watu waliokuwa na silaha walimfyatulia risasi alipokuwa katika ukumbi wake mahususi wa mazoezi lakini kwa bahati nzuri akanusurika jaribio hilo la kutaka kumuua. Amesema baada ya jaribio hilo lililoshindwa la kutaka kumuua alitoa ripoti kwa polisi na kwamba mashahidi waliokuwa karibu pia wamethibitisha jaribio hilo.
Bunge la Bahrain limelaani kitendo hicho kupitia mtandao wake wa intaneti. Kidole cha lawama kuhusu suala hilo kimeelekezwa kwa Khalifa bin Salman, Waziri Mkuu wa Bahrain kwa sababu kabla ya kutekelezwa jaribio hilo, at-Tamimi alikuwa amemkosoa vikali waziri mkuu huyo na kumtuhumu kuwa ndiye aliyesababisha mgogoro wa kiuchumi wa nchi hiyo.
Siku tatu zlizozopita at-Tamimi alimkosoa vikali bungeni Salman kuhusiana na usala hilo na kutaka ajiuzulu na kumwachia mtu mwingine nafasi yake. Alisema chanzo kikuu cha matatizo ya serikali ya Bahrain kinatokana na Waziri Mkuu na hivyo amemtaka ajiuzulu mara moja. 995425