Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Nigeria, Adisna Ishaq mwanachama wa Jumuiya ya Mawakili Waislamu nchini Nigeria ametoa taarifa akisema: 'Mawakili Waislamu nchini Nigeria wanalaani hatua ya utawala wa jimbo la Lagos kupiga marufuku uvaaji Hijabu katika shule za jimbo hilo na watawasilisha malalamiko mbele ya mahakama'.
Ameongeza kupigwa marufuku Hijabu huko Lagos ni katika njama za serikali ya Nigeria kupiga vita Uislamu na Waislamu. Amesema uamuzi wa kuwazuia wasichana wa Kiislamu kuvaa Hijabu shuleni ni uhasama wa wazi dhidi ya Waislamu wa Nigeria na hasa Lagos.
Wakili huyo amesema vazi la Hijabu ni haki ya Waislamu na kuongeza kuwa katika nchi kama Nigeria ambayo waliowengi ni Waislamu, Waislamu wana haki ya kuvaa Hijabu.
Ikumbukwe kuwa karibu asilimia 60 ya watu milioni 160 Nigeria ni Waislamu huku waliosalia wakiwa ni wafuasi wa dini za kijadi na Ukristo.
996088