Mahdi Mustafawi, naibu mkuu anayeshughulikia masuala ya kimataifa katika ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye amesimamia kikao cha siku ya tatu cha 'Mkutano wa Kimataifa wa Dini na Mwamko wa Zama' ameashiria mitazamo ya viongozi wa dini muhimu za mbinguni kuhusiana na suala la mwamko na kongeza kwamba jambo hilo lina umuhimu mkubwa miongoni mwa jamii ya wasomi na wanafikra wa kidini kwa kutilia maanani nafasi muhimu ya dini katika kumkamilisha mwanadamu.
Amesema mazungumzo kati ya dini tofauti yalianza katika baadhi ya nchi kufuatia matukio ya Septemba 11 nchini Marekani ilihali jambo hilo lilianza kuzingatiwa miaka mingi iliyopita katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema mara tu baada ya ushindi wa Mpainduzi ya Kiislamu ya Iran serikali ilianza kutilia mkazo suala la kuheshimiwa itikadi za dini nyinginezo na ushirikiano wa wafuasi wa dini hizo nchini.
Mustafawi ameelezea matumaini yake kwamba mkutano uliotajwa wa kimataifa utasaidia pakubwa katika kuimarisha mwamko katika zama hizi na hatimaye kuchangia katika ukamilifu wa mwanadamu duniani. 998412