IQNA

Waislamu Uingereza watetea nyama halali

23:53 - May 06, 2012
Habari ID: 2319426
Waislamu nchini Uingereza wamepinga vikali pendekezo la kupigwa marufuku uchinjaji kwa njia halali ya Kiislamu.
Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Wales Saleem Kidwai amesema: 'Tunaamini kuwa uchinjaji halali ni hitajio. Aina hii ya uchinjaji huwa ya haraka na yenye kupunguza uchungu.'
Utata kuhusu njia zinazotumiwa na Waislamu kuchinja ulianza wakati Profesa Bill Reilly kiongozi wa zamani wa Jumuiya ya Waganga wa Wanyama Uingereza aliposema uchinjaji unapaswa kupigwa marufuku na badala yake uziraishaji wanyama utumike. Alidai mbinu ya uchinjaji 'Halal' inayotumiwa na Waislamu na uchinjaji aina ya 'Kosher' unaotimiwa na Mayahudi si sahihi.
Kwa mujibu wa mafundishi ya Qur'ani Tukufu, Waislamu wanapaswa kula nyama ya mnyama ambaye amechinjwa shingo kwa kisu baada ya Jina la Allah kutajwa.
Wanazuoni wa Kiislamu wanaafikiana kuwa sheria za Kiislamu zinataka huruma ionyeshwe kwa viumbe wote wa Allah wakiwemo wanyama.
Uislamu pia unawataka Waislamu wawachinje wanyama pasina kuwasababishia uchungu ziada.
Katika fremu ya chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya, baada ya kupigwa marufuku vazi la hijabu, ujenzi wa misikiti na minara ya misikiti, hivi sasa kuna njama za kutaka bidhaa za vyakula halali barani humo zipigwe marufuku.
Marine Le Pen wa Chama cha Kitaifa chenye misimamo mikali huko Ufaransa katika kampeni zake za uchaguzi wa rais alilalamikia kuongezeka chakula halali nchini humo na hivyo kutaka kuwepo vizingiti katika uuzaji wa vyakula halali nchini Ufaransa. Sarkozy vilevile aliunga mkono suala hili lakini si kwa njia ya moja kwa moja.
1001141
captcha