IQNA

Saudia inawapa himaya Mawahabi Pakistan kuwaua Mashia

23:08 - May 07, 2012
Habari ID: 2320529
Kundi la Kiwahabi lenye kufurutu mipaka linaloungwa mkono na Saudi Arabia na Bahrain ndilo linalosababisha mauaji ya kinyama ya Waislamu Mashia huko Pakistan.
"Mauaji hayo yote yanatekelezwa na kundi la Kiwahabi linalojulikana kama Jeshi la Sahaba lililoibuka mwaka 1985 katika mkoa wa Punjab nchini Pakistan kwa lengo la kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waislamu Mashia ambao walikuwa wameanza kupata nafasi katika serikali ya Pakistan,' amesema Ismail Salami mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati katika mahojiano na Press TV.
Ameongeza kuwa, 'Aprili mwaka 2012 pekee, zaidi ya Waislamu Mashia 250 wameuawa na kujeruhiwa hadharani Pakistan.'
Salami ambaye ni mwandishi wa kitabu cha 'Haki za Binaadamu Katika Uislamu' alifafanua kuwa kundi la wanamgambo wa Pakistan lijulikanalo kama Tahrike Taliban (TTP) ni chimbuko kundi la kigaidi la Jeshi la Sahaba.
Salami amedokeza kuwa magaidi wa kundi linalojiita Jeshi la Sahaba wanaungwa mkono na Shirika la Ujasusi la Pakistan na pia linapata himaya ya moja kwa moja kutoka tawala za kifalme za Saudi Arabia na Bahrain ambazo zinaeneza Uwahabi wenye kufurutu mipaka.
1001875
captcha