IQNA

Wanazuoni wa Quds wataka mateka wa Palestina watetewe

12:08 - May 09, 2012
Habari ID: 2322006
Kamati ya Wanazuoni na Wahubiri wa Kipalestina wa Quds Tukufu CPI wamewataka Waislamu na mataifa ya Kiarabu kuwaunga mkono mateka wa Kipalestina wanaosusia chakula katika jela za utawala haramu wa Israel kwa lengo la kulalamikia hali mbaya ya jela hizo.
Kamati hiyo ilitoa taarifa hapo jana Jumanne na kutangaza kuwa, wiki tatu zimepita sasa mbapo mateka hao wanaendelea kugoma kula na watawala wa Israel hawajachukua hatua yoyote ya kutekeleza matakwa yao ya kimsingi kabisa ikiwa ni pamoja na kuwataka wakome kuwazuilia wafungwa katika seli za mtu mmoja na pia kuwafunga bila kuwafikisha mahakamani.
Taarifa hiyo inasema kuwa sababu mbili hizo zimewafanya wachukue hatua ya kususia chakula.
Taarifa hiyo imesema mwishoni kwamba inashangaza kuona kuwa mtu aliyemuua Is'haq Rabin, Waziri Mkuu wa zamani wa utawala haramu wa Israel alifunga ndoa na kufanya harusi akiwa jela na sasa anaishi maisha ya kifahari nje ya jela, na kwamba ndugu yake pia aliyefungwa jela pamoja naye aliachiliwa huru hivi karibuni, lakini maelfu ya mateka wa Kipalestina wanaendelea kuteseka na kufungwa maisha katika jela hizo za kuogofya kwa tuhumu tu kwamba walikuwa wakifikiria njia za kutekeleza operesheni dhidi ya Wazayuni! 1003667
captcha