IQNA

Mkutano wa Qur'ani ya Ahlul Bait kufanyika Pakistan

17:52 - May 09, 2012
Habari ID: 2322443
Mkutano wa Qur'ani na Ahlul Bait utafanyika tarehe 18 Mei katika mji wa Faisalabad nchini Pakistan chini ya usimamizi wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistan.
Mkutano huo utahudhuriwa na maulamaa na wanafikra wa Kishia na Kisuni kwa shabaha ya kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu na kupambana na siasa mbovu za Marekani.
Washiriki katika mkutano huo pia watafanya maandamano ya kupinga kitendo kiovu cha Kasisi Terry Jones wa Marekani cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu. 1003761


captcha