Karibu mateka elfu mbili wa Kipalestina wamekuwa wakisusia chakula tangu tarehe 17 mwezi jana, wakilalamikia siasa za ukandamizaji dhidi ya mateka na wafungwa wa Kipalestina katika jela za utawala haramu wa Israel. Mateka hao wa Kipalsetina wametangaza kuwa, wataendelea na mgomo wako huo hadi pale matakwa yao halali yatakapofikiwa. Wakati huo huo mamia ya mateka wengine wa Kipalestina wametangaza kuungana na wenzao katika mgomo huo wa chakula. Katika hatua ya kufungamana na mateka hao hii leo vijana wa Kipalestina wamefanya maandamano mbele ya ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Ramallah.
Mapema, Shirika la Kimataifa la Hilali na Msalaba Mwekundu lilikuwa limetoa wito wa kufikishwa hospitalini mateka hao wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni.
1003902