IQNA

Waislamu wa Indonesia walalamikia safari ya muimbaji mpotofu wa Marekai nchini humo

12:13 - May 12, 2012
Habari ID: 2323696
Waislamu wa Indonesia wamelalamikia vikali matayarisho ya safari ya mwimbaji wa nyimbo chafu wa Marekani nchini humo.
Waislamu hao wamekemea na kulaani vikali safari ya Lady Gaga ambaye ni mashuhuri kwa kuimba nyimbo chafu na za upotofu nchini Marekani katika nchi hiyo ya Kiislamu. Gaga ametangaza kuwa baadaye mwezi huu atafanya safari nchini Indonesia na kuandaa huko matamasha kadhaa ya muziki, jambo ambalo limewaudhi sana Waislamu na hasa chama cha kutetea Uislamu cha FPI. Sai Munarman, msemaji wa chama hicho ametoa taarifa akisema kuwa Waislamu wa nchi hiyo wamekasirishwa sana na safari ya mwimbaji huyo nchini humo na kuitaka serikali ichukue hatua za haraka kwa lengo la kuifutilia mbali. Amesema mwimbaji huyo ni mwenezaji mkubwa wa fikra za ibada za kishetani na kwamba idadi ya watu wanaoabadu shetani hongezeka kila sehemu anayokwenda. 1004132
captcha