IQNA

' Nadharia ya Mwamko wa Kiislamu kwa mtazamo wa Imam Khomeini MA na Imam Khamenei'

12:30 - May 14, 2012
Habari ID: 2325463
Kongamano la Nadharia ya Mwamko wa Kiislamu kwa mtazamo wa Imam Khomeini MA na Imam Khamenei' limefanyika mjini Tehran Mei 13.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limefunguliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu Wanaomteua Kiongozi Muadhamu Ayatullah Mahdavi Kani na Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu Hujjatul Islam wal Muslimin Mohammadi Golpaygani. Wengine waliohudhuria kongamano hilo ni Imamu wa Muda wa Sala ya Ijumaa Taehran Hujjatul Islam Kadhim Siddiqui pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu kisiasa na kiutamaduni.
Kongamano hilo la siku moja limeandaliwa na Taasisi ya Utafiti na Utamaduni ya Mapinduzi ya Kiislamu (ya kuhifadhi na kuenezza fikra za Ayatullah Sayyed Ali Khamenei).
Mbali na kuchunguza makala teule kongamano hilo pia lilikuwa na vikao maalumu kuhusu fikra za kisiasa za Mapinduzi ya Kiislamu, mkondo wa kihistoria wa mwamko wa Kiislamu na mwamko wa Kiislamu katika uga wa kimataifa.
Karibu makala 350 zilitumwa katika kongamano hilo ambapo makala 60 teule zitachapishwa kwa muundao wa kitabu.
1006341
captcha