Kwa mujibu wa gazeti la Saut al-Balad linalochapishwa Misri. Muungano huo umemtaka Sheikh wa al-Azhar kuchunguza historia ya dhulma na mauaji yaliyofanywa na Mawahabi dhidi ya wafuasi wa Ahlu Beit (as) yaani Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) na kumtaka kukabiliana na itikadi potofu ya Mawahabi inayokufurisha na kuhalalisha damu ya Waislamu wenzao. Taarifa ya muungano huo wa vijana wa Ahlul Beit (as) Imemtaka Sheikh wa al-Azhar na Mufti wa Misri kuvitembelea vituo vya Mashia na kujionea mwenyewe kwa karibu shughuli zinazoendelea huko ili kuthibitisha kwamba shughuli hizo hazihatarishi hata kidogo maslahi ya nchi hiyo bali zinayalinda kutokana na njama za maadui.
Inafaa kukumbusha hapa kwamba jana Jumapili, Sheikh Ahmad at-Tayyib, Sheikh wa al-Azhar alipinga ujenzi wa Husseiniya ya Mashia akidai kwamba jambo hilo litaitenganisha jamii ya Misri! 1012949